Tuesday, 29 November 2016

Mambo manne yatakayokufanya uanze kutumia juisi ya stafeli


Stafeli ni tunda lenye faida lukuki kwa afya ya mwanadamu. Zifuatazo ni faida muhimu za juisi ya tunda hilo.

Huimarisha kinga za mwili.
Juisi ya stafeli husaidia kuimarisha kinga ya mwili kutokana na kuwa na vitamin C yakutosha 

Huboresha mmeng'enyo wa chakula
Tunda hili limeshsheni nyuzinyuzi yaani fiber ambazo pia hupatikana ndani ya juisi yake hivyo matumizi ya juisi hii huweza kuwa suluhisho kwa wale wenye shida ya umeng'enyaji wa chakula.

Huimarisha afya ya mifupa na meno.
Juisi yake ni nzuri kwa afya ya mifupa na meno kwa kuwa imesheheni madini ya phosphorus  pamoja na calcium ambayo yote kwa pamoja husaidia kuimarisha afya ya meno na mifupa mwilini.

Huondoa uwezekano wa kupungukiwa na damu.
Juisi ya stafeli ni nzuri kwa wale wenye anemia kwani inamadini ya chuma ambayo husaidia kutengeneza seli nyekundu za damu.

Kwa maelezo zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment