Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Sunday, 6 November 2016

Mambo matano yatakayokufanya uendelee kuwa na afya bora


Kuwa na afya bora kunahitaji vitu vingi ambavyo visipozingatiwa basi huwa ni rahisi kwa mhusika kusongwa na magonjwa mbalimbali tena mara kwa mara.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ambayo huweza kuchangia mtu kuwa na afya njema;-

1. Mlo kamili 
Binadamu huhitaji kula vyakula vya kujenga mwili, kuupa mwili nguvu na kulinda mwili, ikiwa ni pamoja na matunda, mboga za majani na vyakula vya nafaka hususani ile ambayo haijakobolewa.

Pia usisahau kunywa maji ya kutosha kila siku, huku ukihakikisha unatumia maji safi na salama kabisa.

2. Zingatia Usafi
Kuwa na afya bora huhitji usafi wa mwili , mazingira anayoishi pamoja na vile anavyokula na kunywa. Kwani kuna baadhi ya magonjwa ambayo huchangiwa na mazingira machafu, kwa mfano magonjwa ya kuhara, kipindupindu n.k. Hivyo kudumisha usafi kunaweza kusaida kuepuka magonjwa hayo na mengine yakiwemo yale ya ngozi.

3. Mazoezi
Kufanya mazoezi kunaweza kukusaidia kulala vizuri, kuwa na furaha zaidi, kuwa na uwezo wa kufikiri vizuri , kuwa na mifupa na misuli yenye nguvu, kudumisha au kuwa na uzito wa mwili unaofaa kiafya.

Watu wasiofanya mazoezi huwa katika hatari ya kukumbwa na haufanyi mazoezi magonjwa ya moyo, kisukari pamoja na kiharusi 'stroke'.

4. Pata muda wa kutosha kulala
Usingizi huimarisha mfumo wa kinga na kupunguza hatari ya kupatwa na maambukizo, kisukari, ugonjwa wa moyo n.k

5. Uchunguzi wa afya yako
Ni vizuri kujenga utaratibu wa kuchunguza afya yako mara kwa mara kadri uwezavyo kwani kwa kufanya hivyo husaidia kuweka urahisi kutibu magonjwa yanapokuwa katika hatua za awali.

Kwa mawasiliano zaidi tupigie kwa simu nanmba +255 716 300 200/ +255 784 300 300/ +255 784 300 300.

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

2 comments: