Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 19 November 2016

SIDO yatoa mafunzo ya ukufunzi kwa wajasiriamali

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya viwanda vidogo na biashara, Boniphace Michael (kushoto) akimkabidhi cheti Ndug: Abdallah Mandai (kulia) ambaye ni mmoja wa wakufunzi wa ujasiriamali waliohitimu hivi karibuni
Wizara ya Viwanda na Biashara na Uwekezaji imewataka wajasiriamali kuzitumia malighafi zilizopo nchini kuzalisha bidhaa bora na kuziongezea thamani.

Akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo ya wakufunzi wa usindikaji wa chakula jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na SIDO makao makuu, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya viwanda vidogo na biashara Boniphace Michael, alisema kuwa serikali imedhamiria kutumia malighafi zilizo nchini katika ujenzi wa viwanda ili kuongeza thamani ya mazao ya kilimo hususani ya chakula.

Aidha, Michael alisema kuwa, endapo mazao ya ndani yatatumika ipasavyo itachangia kupunguza upotevu wa mazao usio walazima.

"Takwimu zinaonesha kwamba asilimia 25 hadi 40 za mazao zinapotea na ili kukabiliana na suala hilo ni lazima kuwe na mkakati wa makusudi wa makusudi wa kuongeza thamani ya mazao kwa kuwa na viwanda vidogo na vya kati ambavyo hutumia teknolojia rahisi" alisema Michael.

Hata hivyo, Michael amekiri kwamba suala la mitaji bado ni changamoto kwa wajasiriamali wadogo, lakini serikali imekuwa ikiendelea kulifanyia kazi saula hilo na katika bajeti ya wizara ya mwaka 2016/ 2017 serikali ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 2.4 kwaajili ya kukopesha wajasiriamali.

Pamoja na hayo, Michael alibainisha kuwa serikali imeendelea kufanya mazungumzo na taasisi mbalimbali za kifedha ikiwa ni pamoja na Benk ya TIB ili kuweza kutoa mokopo kwa wajasiriamali ambayo itakuwa na masharti nafuu pamoja na riba nafuu.

Naye Afisa Uendelezaji Biashara SIDO, Jonathan Mbailuka aliwataka wakufunzi waliohitimu mafunzo hayo kutumia vyema ujuzi walioupata kwa kuanzisha viwanda vidogovidogo na kusambaza elimu hiyo kwa watanzania wengine ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Kwa upande wa mmoja wa wahitimu wa kozi hiyo ya ukufunzi, Abdallah Mandai aliipongeza SIDO kwa kuandaa mafunzo hayo na kusema kuwa anayafafananisha mafunzo hayo na barabara iliyonyooka na isiyo na mashimo.

"Kabla ya kupata mafunzo haya ya SIDO naweza kusema nilikuwa  kwenye barabara ya vumbi na baada ya kuhitimu mafunzo haya najihisi nipo kwenye barabara iliyonyooka na isiyonamashimo na ninahisi hata safari yangu ya mafanikio naweza kufika mapema" alisema Mandai

Mbali na hayo, Mandai aliahidi kuitumia elimu hiyo kuwasaidia wajasiriamali wadogo na jamii nzima kwa ujumla katika kujikwamu na changamoto ya umasikini.

Endelea kufuatilia mtandao huu tutakuletea matukio ya picha zaidi kuhusu zoezi la kuhitimisha mafunzo ya wakufunzi lililofanyika Novemba 18/2016 SIDO makao makuu.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300


No comments:

Post a Comment