Monday, 28 November 2016

Ubuyu na faida zake kiafya


Mbuyu ni kati ya miti mikubwa na minene inayopatikana katika ukanda wa tropiki, Matunda yake yanaitwa mabuyu, gamba la tunda hilo huitwa kibuyu na ubuyu ni nyama ya tunda.

Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi. Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.

Mti huu umesheheni malighafi nyingi na nzuri katika afya ya binadamu, ambapo inaelezwa unga wa ubuyu huwa na vitamin na madini mengi, kwani unga huo una kiasi cha vitamin C nyingi kushinda ile inayopatikana kwenye chungwa.

Pia ubuyu una kiwango kingi cha madini ya ‘Calcium’ zaidi ya kile ambacho hupatikana katika maziwa ya ng’ombe, hali kadhalika madini mengine ambayo hupatikana katika ubuyu ni madini ya chuma, magnesium’ na potassium, ambayo nayo hupatikana kwa kiwango kingi zaidi ya ile potassium inayopatika katika ndizi.

Aidha, mti huo wa mbuyu unasifika kwa kutibu magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutibu homa, ambapo mgonjwa atapaswa kuchemsha magome yake na kunywa.

Magome hayo pia husaidia kupunguza madhara kwa watu wenye matatizo ya mfumo wa hewa ikiwa ni pamoja na matatizo ya pumu.

Pamoja na hayo, unga wa ubuyu unapochanganywa na asali husaidia kutibu kikohozi ikiwa mgonjwa atatumia mchanganyiko huo kwa kulamba au kuchanganya na maji ya moto na kunywa.

Mbali na hayo, ubuyu pia huongeza nuru ya macho na kusaidia kuzuia kuharisha na kutapika, huku ukiwa umesheheni madini ya ‘magnesium’, ambayo husaida katika kujenga mifupa ya meno. Hivyo izuri kupata kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa ili kupata faida za ubuyu na utaona matokeo yake mwilini.

Matumizi ya bidhaa zitokanazo na ubuyu pia husaidia kuimarisha afya ya ini kwa sababu ubuyu husaidia sana kuondosha sumu ndani ya mwili na hivyo kuirahisishia ini kufanya kazi zake kwa ufasaha zaidi.

Kimsingi mazao yatokanayo na ubuyu yana faida lukuki, ikiwa ni pamoja na kuimarisha kinga za mwili, kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu, kuboresha afya ya ngozi pamoja na kupunguza hali ya uchovu mwilini.

Malaria ni miongoni mwa magonjwa ambayo huathiri familia nyingi za kiafrika kiuchumi na kijamii, lakini pia ugonjw huo umekuwa ukichangia vifo vya watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano, lakini ni vyema ikafika wakati ikatambulika kuwa kuna miti dawa ambayo huweza kutumiwa kama kinga ya ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na mbuyu.

Ili kutumia mazao ya mbuyu kama kinga ya malaria, utahitajika kupata magome ya mti wa mbuyu na kuyaandaa vizuri kisha kuchemsha na kutumia maji yake kunywa asubuhi na jioni kiasi cha kikombe kimoja kila siku angalau kwa wiki mbili mfululizo hadi mwezi mmoja ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Bidhaa za mbuyu pia husaidia kuulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na saratani pamoja na kukinga dhidi ya upungufu wa damu mwilini kutokana na kuwa na madini chuma ya kutosha zaidi ya kiwango kinachopatikana kwenye nyama nyekundu.

Kwa wenye matatizo ya figo na maumivu ya viungo pamoja na maumivu ya tumbo, mbuyu husaidia pia kukinga na kutibu matatizo hayo ikiwa utatumia bidhaa zitokanazo na mti huu mra kwa mara katika maisha yako ya kila siku.

Ubuyu pia una kiwango cha kutosha cha protini pamoja na nyuzinyuzi, hali ambayo husaidi kupunguza uwezekano wa kukumbwa na matatizo ya ukosefu wa choo.

Hata hivyo, ili kupata manufaa ya mazao haya ya mbuyu ni vyema kutumia ubuyu ulioasili kabisa ambao haujachanganywa na rangi yoyote ili kupata virutubisho vyote vinavyopatikana ndani ya ubuyu.

Pia na wewe unaweza kuuliza maswali yako kupitia inbox yetu ya Facebook ukurasa unaitwa Mandai Products Company Ltd au kwenye email ya dkmandaitz@gamail.com kisha utakuwa ukipata majibu yako kupitia website hii, lakini pia unaweza kutupigia kwa simu 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment