Thursday, 10 November 2016

Yafahamu matunda & viungo yenye uwezo wa kuimarisha afya yako haraka


Picha kwa msaada wa mtandao

Vitamin C ni moja ya virutubisho muhimu ndani ya mwili wa mwanadamu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ukuaji wa miili yetu. Kutokana na hayo vitamin C inaumuhimu katika mlo wetu wa kila siku.

Miongoni mwa kazi za vitamin C mwilini ni pamoja na kuzuia uharibifu wa seli ndani ya mwili pamoja na kupunguza uwezekano wa kukumbwa na saratani za aina mbalimbali na magonjwa sugu.

Pia vitamin C husaidia mwili kumbana dhidi ya maambukizi mbalimbali kama vile kikohozi pamoja na kuimarisha kinga za mwili kwa ujumla.

Je, mwili wako unawezaje kupata vitamin C ?

1. Matumizi ya chungwa.

Chungwa limekuwa likielezwa kuwa na uwezo mzuri wa kuchangia vitamin C ndani ya mwili, hivyo matumizi ya chungwa huweza kuwa moja ya njia nzuri ya kuupatia mwili vitamin C yakutosha.

2. Pilipili

Pilipili nayo inauwezo wa kuongeza vitamin C ndani ya mwili.

3. Nanasi

Tunda hili nalo linakiwango kizuri cha vitamin C, lakini pia tunda hili huweza kupunguza tatizo la ukosefu wa choo na maumivu ya tumbo.

4. Pera

Tunda hili nalo huupatia mwili kiwango kikubwa cha vitamin C pamoja na madini mbalimbali,

5. Peas

Hili nalo ni miongoni mwa matunda ambayo yanaingia kwenye orodha ya matunda yenye kiwango kizuri cha vitamin C.

6. Karafuu

Kiungo hiki nacho ni sehemu ya kiungo chenye vitamin C , hivyo unaweza kutumia ili kupata vitamin hiyo.

7. Embe

Kwanza ni tunda lenye ladha nzuri, lakini pia limesheheni vitamin C yakutosha ndani yake.

Mbali na viyamin C embe pia limesheheni vitamin A, E, B6 pamoja na madini ya copper na potassium.

Zingatia
Tunasema matunda haya yanaweza kukuokoa dhidi ya magonjwa kwa sababu yana vitamin C yakutosha ambayo kazi yake kubwa mwilini ni pamoja na kuimarisha kinga zako za mwili.


Kimsingi yapo matunda mengi yenye kiwango kizuri cha vitamin C ambayo si rahisi kuyataja yote hapa, lakini kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.


No comments:

Post a Comment