Monday, 14 November 2016

Zifahamu faida 4 za mzizi wa mlonge

Mlonge ni mti wenye historia ndefu sana hasa katika masuala ya tiba. Karibu mti wote huu wa mlonge ni dawa. 

Leo nataka kukwambia hizi faida za kutumia mizizi yake ambazo huweza kukusaidia katika kupunguza madhara ya magonjwa kadhaa.

Mizizi ya mti mchanga wa mlonge husaidia kuimarisha afya ya mishipa ya fahamu, kifafa pamoja na tatizo la baridi yabisi sugu.

Mizizi ya mlonge iliyopondwa na kisha kuwekwa chumvi na kubandikwa kwenye uvimbe wowote wa viungo husaidia pamoja na wale waliopooza.

Mtu mwenye maradhi ya koo, pia anaweza kuchemsha mizizi ya mlonge na kutumia maji yake kusukutua.

Hayo ni machache kuhusu faida za mmea huu lakini kwa mengine zaidi unaweza kutupigia simu kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment