Saturday, 17 December 2016

Asali, kitunguu saumu & mafuta ya nazi vinavyoweza kuponya majeraha

Image via Thinkstock
Naamini karibu kila mtu katika maisha yake amewahi kupatwa na jeraha au kidonda, sasa leo napenda kukupatia mbinu kadhaa za asili au ambazo utaweza kuzifanya ikiwa umepatwa na jeraha.

Njia hizo ni pamoja na hizi zifuatazo:-

Asali
Hii ni moja ya mbinu nzuri ya kutibu majeraha na unachotakiwa kufanya ni kupata asali halisi kabisa kisha paka sehemu yenye jeraha asubuhi na jioni kwa muda wa siku 3 hadi wiki utaona mabadiliko.

Kitunguu saumu
Kiungo hiki hutumika pia kama anti- bacterial na ant- fungal hivyo huweza kusaidia kuponya majeraha unachopaswa kufanya ni kupata kitunguu saumu na ukisage kisha tumia rojorojo lake kupaka sehemu yenye jeraha na uiache kwa dakika zisizozidi 10 kisha baada ya hapo toa kitunguu saumu kwenye jeraha. Fanya hivyo asubuhi na jioni kila siku.

Zingatia
Usikae na rojorojo la kitunguu saumu kwenye jeraha kwa zaidi ya dakika 20 na kuendelea kwani huweza kuchangia uharibifu wa ngozi yako.

Mafuta ya nazi
Mafuta haya nayo yanaingia kwenye orodha ya bidhaa ambazo hufanya vizuri kwenye  majeraha unachotakiwa kufanya ni kupata mafuta haya ya nazi halisi kisha pakaza kwenye jeraha na itasaidia kufunga jeraha lako kwa haraka.

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment