Friday, 23 December 2016

Fahamu ukweli kuhusu faida za chungwa na juisi yake

Siku za hivi karibuni nilipokea swali kutoka kwa mmoja wa wasomaji wazuri wa tovuti hii ambaye yeye alipenda kujua kati ya tunda na juisi yake kipi kinamanufaa zaidi kiafya.

Hivyo nikaona ni vyema nimjibu swali lake kwa faida ya wengine pia ambao hupendelea kutembelea tovuti yetu hii.

Kwanza kabisa ifahamike kuwa matunda na juisi asilia, vyote vina manufaa, lakini kimoja kinakuwa bora kuliko kingine kutegemea hali ya mhusika au mtumiaji.

Mfano kwa watu wenye matatizo katika kutafuna wanapotumia juisi ya asilia, huwasaidia kupata virutubisho kwa wingi zaidi katika glasi moja kuliko anapokula tunda likiwa katika hali ya uhalisia wake aambapo huweza kukosa baadhi ya virutubisho kutokana kushindwa kutumia kwa kiwango anachokihitaji.

Kwa mantiki hiyo tunaweza kusema kwamba juisi hufaa zaidi kwa mgonjwa ambaye mara nyingi meno yake hayawezi kutafuna vizuri na mahitaji ya nishati ya mwili wake ni makubwa.

Aidha, juisi hasa iliyotengenezwa na matunda halisi bila ya kuwekwa sukari au yenye sukari kidogo ni kinywaji kizuri na kina faida kubwa kwa wagonjwa kuwasaidia kuwa na afya bora.

Pamoja na hayo juisi inaongeza maji mwilini, lakini pia zaidi ya hayo, juisi za matunda na mbogamboga zinamsaidia mwili kuondoa sumu mwilini kupitia haja ndogo

Mbali na hayo, upande wa ulaji wa matunda kwa kutafuna nao huwa na manufaa yake zaidi kwani husaidia kupata virutubisho vyote vya tunda husika. Hii ni kutokana na mchakato wa kutengeneza juisi ambao huchangia baadhi ya virutubisho muhimu kuharibika au kupotea kutokana n kuonekana kuwa ni uchafu na kutupwa.

Baadhi ya matunda ngozi zake zinaweza kuliwa na ni chanzo muhimu cha virutubisho ikiwa ni pamoja na nyuzinyuzi yaani 'fiber' ambazo huenda kuboresha mfumo wa umeng'enyaji tumboni na hivyo kupunguza uwezekano wa tatizo la kukosa choo.

Pamoja na faida hiyo ya kula tunda halisi pia faida nyingine ni kuongeza shibe kwa mhusika. Ulaji wa matunda humsaidia mhusika kuhisi shibe, lakini juisi huleta shibe ya muda mfupi na kuongeza nishati mwilini kwa haraka.

Pia kama unapenda juisi halisi yenye virutubisho vya kutosha unaweza kufika Mandai Natural Food iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam utapata juisi hiyo iliyoandaliwa kitaalam na kuzingatia taratibu zote za kiafya.

Kwa maelezo zaidi na ushauri tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

2 comments: