Friday, 30 December 2016

Faida 3 muhimu kuhusu mboga za majani ndani ya familia yako


Mboga za majani nimoja ya bidhaa ambazo zimekuwa zikipigiwa chapuo na watu wengi hususani wataalam wa afya kutokana na  umuhimu wake mwilini

Hapa ninazo faida kadhaa za ulaji wa mbogamboga kwenye familia yako;-

1. Mboga za majani husaidia kupunguza sumu inayozalishwa na vyakula  au vinywaji vingine ndani ya mwili.

2. Mboga hizi za majani pia ni moja ya chanzo kizuri cha vitamin C ambayo ni muhimu mwilini kutokana na kuimarisha kinga za mwili.

3. Ulaji wa mboga za majani pia husaidia kuongeza kirutubisho cha carotene ambayo hubadilishwa mwilini na kuwa vitamin A hivyo matokeo yake huenda kusaidia pia afya ya macho.

Kwa maelezo zaidi na ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

1 comment:

  1. http://nhlwinterclassic2017.us/
    http://nhlwinterclassic2017.us/
    http://nhlwinterclassic2017.us/

    ReplyDelete