Wednesday, 21 December 2016

Faida 5 muhimu atakazopata mamamjamzito anayekula tikitimaji mara kwa maraTIKITIMAJI ni moja ya matunda yanayolimwa sana katika maeneo mbalimbali nchini tofauti na miaka iliyopita.

Hali hiyo inaashiria kuwa tunda hilo linawatumiaji wengi, huenda ni kutokana na faida zake au ladha yake nzuri.

Tunda hili kisayansi linajulikana kama ‘Citrullus lanatus’ na ukuaji wake huwa ni wa kutambaa.

Lina umbo linalofanana na tufe au yai. Asili ya tunda hili ni Afrika Magharibi na Kusini.

Inakadiriwa kuwa asilimia 92 ya tunda hili ni maji, lakini licha ya kuwa na maji hayo yenye ladha nzuri pia hili faida kadhaa katika masuala ya afya hususan pale linapotumika ipasavyo.

Tikitimaji ni chanzo cha virutubisho mbalimbali ndani ya mwili wa mwanadamu ikiwa ni pamoja na vitamin A ambayo husadia kuimarisha afya ya macho.

Leo napenda tufahamishane zaidi kuhusu umuhimu wa tunda hili kwa mamamjamzito.
Hupambana na mfumo mbovu wa umeng’eji chakula tumboni
Mara nyingi mwanamke anapokuwa mjamzito huweza kukumbwa na tatizo la kukosa choo, lakini matumizi ya tunda la tikitimaji hasa juisi yake huweza kuwa suluhisho la tatizo hilo.

Matumizi ya tikitimaji pia husaidia kuzuia tatizo la mwili kuvimba
Wanawake wengi wanapokuwa katika hali ya ujauzito baadhi yao hupatwa na matatizo ya miguu kuvimba au mikono, hivyo matumizi ya tikitimaji huweza kutatua tatizo hilo kutokana na tunda hilo kuwa na madini ambayo huweza kuzuia mishipa ya damu isizibe.

Tikitimaji pia husaidia kupambana na homa za asubuhi ‘Morning sickness’
Inaelezwa kuwa tunda hili ni nzuri kwa wanawake wajawazito kwani husaidia kuzuia kichefuchefu hususani asubuhi, Tikitimaji huwa na nafasi kubwa ya kutuliza hali ya kichefuchefu hivyo kwa wanawake ambao hukumbwa na hali hiyo ni vyema kutumia tunda hili.

Tikitimaji pia husaidia kuzuia upungufu wa maji mwilini
Tunda hili husifika kwa kuwa na kiwango kikubwa cha maji, hivyo hufaa kwa wanawake hususani wanapokuwa katika hali ya ujauzito.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba +255 716 300 200/ +255 769 400 800/ +255 784 300 300 au Barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment