Saturday, 3 December 2016

Ganda la chungwa na manjao huweza kumaliza chunusi ndani ya wiki 1


Tatizo la chunusi ni moja ya matatizo ambayo huwasumbua watu wengi na hasa vijana na wengi wao wakijikuta wakitumia muda mwingi pamoja na gharama kubwa katika kukabiliana na tatizo hilo.

Hapa ninayo mbinu mbadala na rahisi kwako ambayo huweza kusaidia kumaliza tatizo la chunusi endapo itatumika ipasavyo.

Mbinu yenyewe ni hii ya kutumia maganda ya chungwa pamoja na unga wa manjano.

Unachopaswa kufanya ni kuyakausha maganda ya chungwa kisha yasage na upate unga wake halafu utachanganya na unga wa manjao na kupata mchanganyiko wa pamoja.

Jinsi ya kutumia mchanganyiko huo utaweka kwenye bakuri na kuchanganya na maji kidogo sana kisha paka usoni au sehemu zenye chunusi halafu utakaa nao kwa dakika 20 kisha nawa kwa maji uvuguvugu. Fanya zoezi hilo ndani ya wiki na utajionea mabadiliko.Kwa maelezo zaidi au ufafanuzi kuhusu mbinu hii unaweza kutupigia kwa simu kwa namba: 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.
No comments:

Post a Comment