Friday, 9 December 2016

Hii ni kwa wale wapenzi wa nyama, haya ndio madhara yake


Naamini huenda utakuwa umewahi kusikia baadhi ya wataalam wa afya wakizungumza kuhusu madhara yanayoweza kuwapata watumiaji wa nyama nyekundu.

Kama hukuwahi kusikia basi napenda kukumbusha kuwa ulaji wa nyama nyekundu kupita kiasi au mara kwa mara ni hatari kwa afya yako.

Awali ya yote huenda baadhi ya watu wanaweza kuwa hawaelewi nyama nyekundi ni ya aina gani. Mfano wa nyama nyekundu ni pamoja na ile ya ng'ombe na mbuzi n.k

Leo napenda kukwambia moja ya hatari ya kutumia nyama nyekundu mara kwa mara.
Ulaji wa nyama nyekundu mara kwa mara kwa mara unaweza kusababisha figo kushindwa kufanya kazi zake ipasavyo mwilini tatizo hili hufahamika kama 'kidney failure'

Inaelezwa kuwa walaji wa nyama nyekundu huwa katika hatari ya kupatwa na tatizo hilo kwa kiwango cha  asilimi 40 na hivyo kufanya figo kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo ndani ya mwili. 
 
Hata hvyo, wakati tukielezana kuhusu madhara ya nyama nyekundu basi tunashauriwa kutumia nyama nyeupe 'white meat' ambayo ni ile kuku au samaki.

Kwa maelezo zaidi au ufafanuzi kuhusu matumizi ya lishe na ulaji bora unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment