Monday, 12 December 2016

Hiki ndio kiungo chenye ladha nzuri kwa chakula na faida lukuki kiafya


Vipo viungo kadhaa ambavyo husifika kwa kuongeza ladha ya chakula pamoja na muonekano mzuri pia.

Miongoni mwa viungo hivyo ni pamoja na hoho, lakini kiungo hiki hakiishii tuu kuongeza ladha pamoja na kubadili muonekano wa chakula bali pia husaidia baadhi ya mambo ndani ya miili yetu.

Ninazo hapa faida kadhaa za hoho kiafya ni vyema ukazifahamu hapa;

Kwanza husaidia kupunguza uwezekano wa kupatwa na matatizo ya tezi dume, hii ni kutokana na kuwa na vitamin C, E, A ambavyo vyote kwa pamoja husaidia kumuepusha mhusika dhidi ya matatizo hayo.

Hoho pia husaidia kuboresha mifupa kutokana na kuwa na kiwango cha vitamin C ya kutosha hasa unapotumia hoho ile ya rangi nyekundu au njano.

Aidha, kiungo hiki kinauwezo wa kusaidia kupunguza uzito na kuwasaidia wale wenye shida ya anemia kwa sababu ina vitamin C yakutosha ambayo husaidia kunyonya madini ya chuma.

Kwa maelezo zaidi au ufafanuzi kuhusu matumizi ya lishe na ulaji bora unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

1 comment: