Friday, 16 December 2016

Jinsi hali ya upweke inavyoweza kuharibu afya yako ikiwa utakosa msaada

Upweke ni ile hali ya kuhisi uko peke yako wakati pale unapohitaji campan au watu wa karibu wa kushirikiana nao kwa mawazo au furaha. 

Inapotokea mtu yupo peke yake na ameridhika na hali hiyo huo sio upweke tena lakini tatizo huja pale anapoona kuna kitu kimepungua na yuko peke basi hali hiyo ndiyo huleta upweke. 

Kuna wakati mtu huamua kukaa peke yake labda kwa kutafakati mambo mbalimbali na kukaa mbali na makelele au fujo.

Zipo athari kadhaa za tatizo hili la upweke kama ifuatavyo:-

1. Hali ya upweke huweza kushusha uwezo wa kinga na mwili na hivyo kuongeza nafasi ya kupata magonjwa mbalimbali kirahisi.

2. Pia hali ya upweke huweza kuwa chanzo cha matatizo yanayohusiana na moyo.

3. Hali ya upweke pia hupelekea kufanya maamuzi mabaya kama vile kujiingiza kwenye ulevi, ngono, unyang'anyi, uvutaji sigara n.k yote hayo hufanywa na mhusika kutokana na kuhisi ni njia ya kuondoa hali hiyo kumbe sivyo.

Kimsingi tatizo hili linanafasi kubwa ya kuathiri maisha ya mwanadamu.

Endelea kufuatilia tovuti hii kwani baadaye nitakuletea jinsi ya kumaliza tatizo hili.

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment