Thursday, 15 December 2016

Kitunguu swaumu & mbegu za maboga vinatosha kumaliza tatizo la maumivu ya kiuno


Maumivu ya kiuno ni hali inayotokea mara nyingi kwenye kiwiliwili cha misuli na inayohusu misuli na mifupa ya upande wa chini wa mgongo.

Hali hiyo inaelezwa huathiri takriban asilimia 40 ya watu wakati fulani wa kipindi cha maishani mwao.

Maumivu hayo huweza kugawanywa kwa pande mbili yale yanayodumu kwa kipindi cha chini ya wiki 6 na maumivu sugu ya wastani (wiki 6 hadi 12), au maumivu sugu (zaidi ya wiki 12). Hali hii pia inaweza kuainishwa kulingana na visababishi kama inayosababishwa na jeraha isiyosababishwa na jeraha au maumivu mengine.

Kuna njia nyingi mbadala katika watu ambao wasiopata nafuu baada ya matibabu ya kawaida, njia hizo ni pamoja na matumizi ya kitunguu swaumu pamoja na mbegu za maboga

Kitunguu swaumu, huweza kutumika baada ya kusagwa na ile rojorojo yake itatumika kwa kuchua sehemu yenye kiuno ambayo inamaumivu. Fanya zoezi hilo angalau mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni.

Kuhusu mbegu za maboga, unatakiwa usage kisha tumia unga wake kwa kuchanganya kwenye uji mwepesi halafu kunywa asubuhi na jioni kila siku.

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment