Friday, 16 December 2016

Kuandika malengo kunavyoweza kurahisisha maisha yako


Kuna umuhimu mkubwa sana katika kuandika malengo kwenye karatasi. ikiwa ni pamoja na kutengenezea saikolojia ya kuwa una malengo na malengo yako ni ya muhimu. 

Hivyo, hakikisha unaandika malengo yako na unayasoma mara kwa mara huku ukijikumbushia na amini kuwa utayatimiza. Pia usiache kujituma katika njia yoyote ili kuweza kutimiza malengo yako.

Tafiti zinaonesha  kuwa asilimia 78% ya watu ambao wameandika malengo yao kwenye karatasi hufanikiwa kutimiza malengo yao na asilimia ndogo iliyobakia ni wale ambao hawakuandika malengo yao kwenye report lakini nao kuna wakati huweza kufanikiwa japo si mara zote.

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment