Tuesday, 27 December 2016

Mambo matatu muhimu kuhusu boga kwenye ngozi zetu

Boga ni mojawapo ya tunda zuri na lenye virutubisho vingi ambavyo vyote ni muhimu sana kwa afya ya miili yetu.

Kama utakuwa ni mfuatiliaji wa masomo yetu a kwa mara kupitia tovuti hii nadhani utakuwa unakumbuka kuwa mara kadhaa tumeshazungumza kuhusu faida za boga kwa ujumla, lakini hiyo haizuii kuendelea kuzungumzia sifa za boga leo tena.

Leo napenda tuzungumzie uwezo wa boga katika kuboresha afya ya ngozi zetu kama ifuatavyo>>
Kwanza kabisa unapotumia boga husaidia kuleta unyevunyevu kwenye ngozi na hivyo kuwasaidia wale wenye ngozi kavu hii ni kutokana na kuwa na vitamin E ya kutosha pamoja na kirutubisho kiitwacho 'antioxidant '

Maboga pia yana vitamin A yakutosha ambayo husaidia kulinda ngozi dhidi ya kuharibika na kuunda seli mpya ndani ya ngozi.

Lakini pia ndani ya boga kuna vitamin C ambayo nayo huhitajika  katika kuhakikisha afya ya ngozi inakaa vizuri zaidi siku zote

Hayo ni machache kuhusu afya ya ngozi na matumizi ya boga, lakini kwa mengine mengi unaweza kuwasiliana na Mtaalam  Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.


No comments:

Post a Comment