Sunday, 25 December 2016

Mambo matatu muhimu unayopaswa kufanya kila asubuhi unapoamka
Sala
Mara unapoamka jitahidi kusali, kwani ni muhimu kufanya hivyo katika maisha kwa sababu naamini kila mtu anaamini uwepo wa Mungu.

Unaposali unamaanisha kuwa unatambua na kushukuru kwa nafasi uliyoipata katika maisha yako. shukrani ni kitu kikubwa sana ambacho hivyo ni vyema kufanya hivyo mara unapoamka tu.

Jitathimini kuhusu malengo yako
Jenga utamaduni wa kusoma mara kwa mara malengo yako ambayo umeyaandika ili kuweza kujikumbusha na kujua unatakiwa kufanyanini. Hivyo unayokila sababu ya kukumbuka kusoma mara kwa mara malengo yako.

Mazoezi
Jitahidi utenge angalau dakika 30 tu kila siku za kufanya mazoezi ya viungo ili kuimarisha afya yako na kuuweka mwili fit zaidi.

Kwa maelezo zaidi na ushauri tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment