Saturday, 17 December 2016

Orodha ya mambo matano ambayo yatakufanya ubaki na afya bora


Nahakika hakuna mtu ambaye anapenda kuzongwa na magonjwa, kila siku au kila mwezi, bila shaka kila mtu angependa kuwa na afya bora maisha yake yote ili aweze kutimiza malengo yake ya kimaisha.

Ndio maana kuna ule usemi usemao 'bora kinga, kuliko tiba' hivyo na mimi leo napenda kukwambia mambo matano muhimu yatakayokufanya uepuke magonjwa yasiyoyalazima mara kwa mara.

1. Kuwa muangalifu na chakula unachokula kila siku, hakikisha ni salama kwa afya yako na kinavirutubisho muhimu karibu vyote.

2. Zingatia kunywa maji ya kutosha kila siku, kwani ni moja ya vitu muhimu ndani ya miili yetu.

3. Zingatia usafi katika mazingira yako, hii ni pamoja na usafi wa mwili wako, mavazi, chakula pamoja na mazingira yako ya kila siku.

4. Fanya mazoezi kila siku angalau dakika 30 kila unapopata muda wa kufanya  hivyo.

5. Pata muda wa kulala wa kutosha angalau zisipungue japo saa 8 ili kuupatia mwili muda mzuri pia wa kupumzika.

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment