Tuesday, 6 December 2016

Usipitwe na haya mambo muhimu kuhusu kitunguu maji


KITUNGUU maji ni moja ya kiungo ambacho hutumika karibu kila siku katika mapishi, lakini kiungo hiki pia kina nafasi yake katika kutuliza matatizo mbalimbali kiafya.

Miongoni mwa faida za kitunguu maji ni pamoja na hizi zifuatazo:-

Husaidia kupunguza matatizo ya homa pamoja na matatizo ya koo.

Pia kitunguu maji huweza kusaidia kupunguza shida ya kutokwa na damu puani

Aidha, mbali na hayo, kiungo hiki huweza kuboresha mmeng'enyo wa chakula tumboni, hivyo kama unatatizo hilo unaweza kutumia kiungo hicho.

Pamoja na hayo, kitunguu maji husaidia kushusha cholesterol ndani ya mwili.

Mbali na hayo, kiungo hiki husaidia kupunguza maumivu ya viungo ndani ya mwili.

Pia unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment