Friday, 16 December 2016

Uwezo wa kitunguu maji kwa wenye maumivu ya sikio

Sikio pua na koo ni viungo vinavyohusiana kwa ukaribu sana kiasi kwamba linapotokea tatizo katika kiungo kimojawapo, tatizo hilo pia huweza kujitokeza pia katika kiungo kingine.

Mfano inapotokea pua zimeziba, basi masikio pia yanaziba au sikio linapouma pia pua huweza kutoa kamasi hali kadhalika na koo linapouma wakati wa kumeza chakula sikio pia linauma.


Miongoni mwa sababu zinazoweza kusababisha maumivu ya sikio ni pamoja na uwepo wa jipu au upele ndani ya njia, kelele za nguvu, kupenga kamasi kwa nguvu, kukaukiana kwa nta ndani ya sikio n.k.

Mara nyingi maumivu mengi ya sikio huwa yanakubali matibabu kwa urahisi, isipokuwa ni vyema kwanza kupata ushauri kutoka kwa wataalam kwanza.

Zipo njia mbalimbali za kupunguza maumivu ya sikio linapokuwa na maumivu, lakini kwa leo nitakufahamisha hii ya kutumia kitunguu maji ambacho ni rahisi hata kukipata katika mazingira yetu ya kila siku.

Unachopaswa kufanya ni kuchukua kitunguu maji kisha tengeneza juisi yake na baadaye utatumia matone mawili hadi matatu katika sikio.

Fanya hivyo, mara tatu kwa siku kwa muda wa siku tano, Tiba hii ni mahususi kwa sikio linalouma au ambalo limeziba kutokana na kujaa nta.

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa, ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment