Monday, 30 January 2017

Aina 10 ya vyakula unavyopaswa kula wakati unapokuwa kwenye siku zako (period)Katika kipindi cha mzunguko (siku za hedhi) kwa kawaida wanawake hupoteza kiasi cha damu pamoja na baadhi ya madini mwilini.

Hali hiyo huweza kusababisha upungufu wa damu kama mwanamke atakuwa hapati lishe bora na ya kutosha. Sasa ili kuzuia upungufu wa damu na madini mwilini, msichana anatakiwa kula vyakula vyenye madini chuma na chokaa kwa wingi ikiwa ni pamoja na hivi vifuatavyo:-

Orodha ya vyakula vinavyopendekezwa

1. Mboga za majani
2. Maharage
3. Soya
4. Samaki
5. Maziwa
6. Korosho
7. Mayai
8. Zabibu (Juisi yake)
9. Matunda damu
10. Dagaa n.k.

Mbali na vyakula hivyo, pia mwanamke huhitaji kunywa maji ya kutosha kipindi hiki na kuzingatia hali ya usafi wa mwili, hasa sehemu za siri . Tumia vitambaa safi vilivyo nyooshwa kwa pasi au pedi zilizohifadhiwa katika hali ya usafi.

Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 769 400 800, +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.
Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment