Friday, 20 January 2017

Aina 4 za matunda ambayo unapaswa kula angalau kila siku


Ukweli ni kwamba kuna aina ya matunda mbalimbali lakini kila tunda huwa na sifa zake kiafya.

Hapa ninayo orodha ya matunda ambayo yanashauriwa kuliwa mara kwa na kuwa na faida ndani ya mwili.

1. Tufaa/ apple.
Hili ni tunda ambalo lina kiwango kizuri cha fiber, lakini pia tunda hili lina vitamin C .

2. Parachichi

Hili ni tunda ambalo lipo tofauti sana na matunda mengine kutokana na kuwa na aina ya mafuta asili yenye kuleta afya mwilini pamoja na vitamin C na fiber.

3. Ndizi
Hili ni moja ya tunda lenye thamani pia kwani limesheheni madini ya potassium pamoja na vitamin B6 na fiber pia.

4. Chungwa.

Tunda hili limekuwa likifahamika zaidi kwa kuwa na vitamin C nyingi na hivyo kuimarisha kinga za mwili zaidi.

Unaweza kujitahidi kupata tunda moja kila siku kati ya hayo hapo juu kila baada ya mlo wako ili kujenga afya yako zaidi.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment