Saturday, 21 January 2017

Aina 5 ya vyakula vya kuepuka wakati wa kunyonyesha


Wakati wa mama anaponyonyesha huwa ni wakati muhimu sana kwa mtoto na ni moja zoezi ambalo huhitaji umakini mkubwa huenda kuliko wakati mwingine kwani hapo tunakuwa tunazungumzia afya ya mtoto ambaye kwa kiasi kikubwa hutegemea chakula kutoka kwa mama pekee.

Yapo mambo kadhaa ambayo hupaswa kuzingatia wakati wa unyonyeshaji ikiwa ni pamoja na kuzingatia hali ya usafi.

Hapa ninayo orodha ya vyakula vya kuepuka wakati wa unyonyeshaji.

1. Mwanamke anayenyonyeshwa hushauriwa kuepuka matumizi ya kahawa kutokana na kuwa na kiwango cha caffeine.

2. Epuka matumizi ya matunda yenye uchachu sana kama vile limao au ndimu na badala yake unaweza kula zaidi mapapi au embe.

3. Mwanamke anayenyonyesha hupaswa kuepuka unywaji wa pombe kwani huweza kuleta madhara kwenye afya ya mtoto.

4. Matumizi ya vyakula vyenye viungo vingi pia haishauriwi kwa wanawake wenye kunyonyesha.

5. Kitunguu swaumu  pia si kizuri kwa mama anayenyonyesha kwani huweza kuchangia madhara kwa mtoto pia kupitia maziwa.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment