Thursday, 12 January 2017

Dalili hizi zinaashiria matatizo ya uzazi


Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi ni tatizo ambalo linaweza kumpata mwanamke yeyote.

Kwa kawaida mimba hutunga ndani ya mfuko wa kizazi isipokuwa mara chache huweza kutokea nje ya eneo hili maalumu.

Katika nyumba ya uzazi kuna mirija inayoitwa fallopian ambayo kazi yake ni kusafirisha mayai kutoka katika kiwanda chake cha uzalishaji; ovari hadi kwenye mfuko wa uzazi. Hapo ndipo mimba inapaswa kutokea.

Kwa bahati mbaya ama kutokana na hitilafu fulani mimba hiyo inaweza ikatungishiwa kwenye moja ya mirija miwili ya kizazi; upande wa kulia au kushoto.

Ikitokea hivyo, basi itafahamika kuwa mimba hiyo imetungwa nje ya kizazi. Vilevile mimba inaweza ikawa imetungwa nje ya nyumba ya uzazi au mirija.

Mimba zinazotungwa kwenye fallopian husababisha misuli inayozunguka mirija hiyo kushindwa kufanya kazi kutokana na mgandamizo wa mimba inavyokua. Hali hiyo husababisha mishipa inayopita karibu na fallopian kupasuka na damu kutoka kwa wingi hali ambayo isiposhughulikiwa haraka huweza kusababisha madhara zaidi na hata kifo kwa mama.

Tatizo hili huwa halina chanzo cha moja kwa moja, lakini kuna baadhi ya viashiria ambavyo ni pamoja na magonjwa kama maambukizi katika mfumo wa uzazi hasa yale yanayosababisha uvimbe.

Mambo mengine yanayoweza kusababisha mimba kutungwa nje ya nyumba ya uzazi ni uvutaji wa sigara. Kutokana na nikotini iliyoko ndani ya tumbaku kuchochea kusinyaa kwa mirija ya fallopian na hata kusababisha mirija hiyo kuziba.

Jambo jingine ni upasuaji wa tumbo uliofanyika zamani unaohusu mirija ya fallopian na kusababisha mrija husika kusinyaa.

Dalili za tatizo hili mara nyingi huanza kujitokeza kati ya wiki sita hadi nane baada ya mwanamke kuona hedhi kwa mara ya mwisho.

Hata hivyo, mwanzoni mwa ujauzito hususani katika wiki ya kwanza, mimba iliyotunga nje ya mfuko wa kizazi huwa na dalili sawa na zile za mimba iliyotungwa eneo la kawaida.

Hivyo ni vigumu kujua mimba iliyotungwa nje ya mfuko, licha ya kuwa inaweza kuchochea kupata kichefuchefu na kuishiwa nguvu, lakini dalili hizi piahuweza kuwapata pia wale ambao mimba zimetungwa eneo la kawaida.

Mara zote huwa inashauriwa mama mjamzito kwenda kliniki mapema angalau katika kipindi kisichozidi miezi mitatu, na ikiwa atabainika kuwa na shida hiyo aweze kuhudumiwa.

Mama anapochelewa hadi mimba ikafikia miezi sita hadi nane, huwa tayari mirija ya uzazi imeshazidiwa na hivyo kushindwa kuhimili kuubeba ujauzito, hivyo humfanya mwanamke kupata maumivu makali chini ya nyonga, kuhisi kizunguzungu,shikizo la damu kushuka na damu kutoka ukeni.

Maumivu huwa ni makali sana kwa mwanamke mfano wa kisu kinapokata na yanaweza kuwa ni ya upande mmoja wa nyonga .

Tatizo hili huweza kutibiwa kwa namna mbili,yaani upasuaji au kutumia dawa, lakini endapo mirija itakuwa tayari imeshapasuka basi upasuaji wa dharura hufanyika kwa ajili ya kuzuia kupoteza kwa damu zaidi.

Pia na wewe unaweza kuuliza maswali yako kupitia inbox yetu ya Facebook ukurasa unaitwa Mandai Products Company Ltd au kwenye email ya dkmandaitz@gamail.com kisha utakuwa ukipata majibu yako kupitia website hii, lakini pia unaweza kutupigia kwa simu 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment