Saturday, 7 January 2017

Epuka kutumia kiungo hiki kama unamatatizo ya vidonda vya tumboKama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa tovuti yetu naamini utakuwa unafahamu kuwa mara kadhaa tumekuwa tukizungumzia kuhusu mimea tiba pamoja na viungo mbalimbali.

Sasa leo naomba nikueleze ni watu wa aina gani hawapaswi kutumia kiungo cha tangawizi licha ya kwamba ni kiungo ambacho kinafaida nyingi za kiafya.

Kabla ya yote kumbuka kuwa waswahili husema kila kitu huwa na faida na hasara zake sasa hizi zifuatazo tunaweza kusema kama ni hasara za kutumia tangawizi kwa baadhi ya watu.

Kwanza kabisa kama utakuwa na tatizo la vidonda vya tumbo basi tambua huruhusiwi kutumia kiungo hiki, kwani utakapofanya hivyo huweza kupelekea kuongezeka kwa madhara zaidi.

Pili wale wenye tatizo la kutokwa na damu mara kwa mara, hii ni kwa sababu tangawizi huweza kuchangia  kuhamasisha mzunguko wa damu ndani ya mwili kuwa mkubwa zaidi.

Kikombe cha chai yenye tangawizi
Tatu wale wenye shida ya kiungulia nao wanapotumia tangawizi huweza kuchangia kuongezeka kwa hali hiyo, hivyo kama unahali hiyo ni vyema ukaepuka matumizi ya kiungo hiki.

Pamoja na hayo, matumizi ya kiungo hiki huweza kuchangia kuwashwa kwa kinywa.

Hivyo basi ikiwa unahitaji kutumia kiungo hiki kwa kupata faida za kiafya ni vyema kufanya mawasilianao na wataalam wa masuala ya mimea tiba ili kupata ufafanuzi zaidi. Au tupigie sisi moja kwa moja na tutakusaidia kukupatia ufafanuzi zaidi juu ya kiungo hiki.

Unaweza wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment