Saturday, 21 January 2017

Je, unafahamu kiazi mviringo kinaweza kukuondoa kwenye vidonda vya tumbo?


Mara nyingi tumekuwa tukitumia viazi mviringo kama chakula ambacho huweza kupikwa au kutengenezwa kwa namna mbalimbali kutokana na uhitaji wa mhusika. Mfano chips.

Hata hivyo, licha ya kwamba viazi hutumiwa mara kwa mara, lakini wengi hawafahamu zaidi kuhusu faida zake

Leo nimeona nikwambie hizi faida kadhaa za viazi mviringo kwako:-

Viazi mviringo vikipondwa na kubandikwa juu ya tatizo lolote la ngozi husaidia kupunguza tatizo hilo au kumaliza kabisa endapo njia hiyo itatumika mara kwa mara.

Pamoja na hayo, kiazi kinapopondwa na kupatikana juisi yake huweza kusaidia kwa wale wenye matatizo ya baridi yabisi na vidonda vya tumbo.

Hali kadhalika, kiazi pia ni ‘tonic’ nzuri sana ya ngozi, kinachotakiwa kufanyika katika hili ni kunawia juisi yake na machicha yake utayabandika kila mahali juu ya ngozi na itasaidia kuondoa makunyanzi yote ya uzee pamoja na kulainisha ngozi.

Kwa maelezo zaidi na ushauri tupigie kwa namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment