Monday, 30 January 2017

Je, unafahamu korosho hulinda afya ya moyo? majibu yapo hapa


Habari za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com sina shaka unaendelea vyema,kama utakuwa haupo sawa kiafya naomba nikupe pole na unaweza kuwasiliana nasi kwa msaada zaidi kwa namba hapo chini, lakini kwa sasa naomba kuwasilisha kwako hizi faida za korosho.

Korosho ni moja ya zao la biashara ambalo hupatikana sana Kusini mwa Tanzania, Mtwara, licha ya kwamba zao hili linafahamika sana kama zao la biashara, lakini bado zao hili lina faida kwa afya zetu pia.

Baadhi ya faidi za matumizi ya korosho kama ifuatavyo:
Matumizi ya korosho yanasifika sana kwa kuwa na uwezo wa kulinda afya ya moyo kutokana na kwamba korosha ndani yake inakirutubisho kiitwacho 'antioxidants'.

Aidha, korosho pia inasifika kwa kuwa na madini ya 'magnesium' ambayo husaidia kuimarisha afya ya mifupa na meno, lakini pia humsaidia mhusika anayependelea kutumia korosho kuwa na nafasi ndogo ya kupatwa na matatizo ya shinikizo la damu, hususani shinikizo la juu la damu.

Pia ulaji wa korosho husaidia sana kuimarisha afya ya usingizi na kumfanya mhusika kuacha kupata usingizi wa mang'amng'am na badala yake atajikuta akipata usingizi mzuri kabisa.

Mara nyingi kinamama wanaoingia kwenye kufungu hedhi 'menopause' wao huzongwa sana na tatizo la kukosa usingizi, hivyo wanashauriwa kutumia korosho ili kuepuka tatizo hilo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 769 400 800, +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment