Monday, 16 January 2017

Je,unajua kwa siku unatakiwa kupata choo mara ngapi? majibu yapo hapa

Kwa kawaida mtu mwenye afya nzuri huhitajika kwenda chooni angalau mara tatu kwa siku. Jambo ambalo wengi huwa halijitokezi kwao na wengi huona hali ya kawaida kabisa.

Zipo sababu ambazo huchangia tatizo hili la kukosa choo ikiwa ni pamoja na ulaji wa vyakula hasa vile visivyokuwa na asili ya nyuzinyuzi.

Pia tatizo hili huweza kuchangiwa na kutokuwepo na mazingira rafiki ya kupata haja yaani choo au choo kutokuwa na miundombinu mizuri au mizuri lakini haipo katika hali ya usafi wa kumshawishi mhusika kwenda kupata haja.

Zifuatazo ni sababu nyingine ambazo huchangia tatizo la kukosa choo :-

1. Kushindwa kunywa maji mengi

2. Kushindwa kupata vyakula visivyokuwa na 'fiber' yaani nyuzinyuzi.

3. Ulaji wa nyama nyekundu kupitiliza

4. Ukosefu wa mazoezi ya mwili.

Kwa maelezo zaidi au ushauri unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment