Friday, 6 January 2017

Kama si mpenzi wa bamia, basi tambua unapitwa na faida hizi kiafyaBamia ni mboga ambayo inafahamika na watu wengi hasa watanzania na imekuwa ikitumiwa na watu wengi hapa nchini.

Pamoja na kuwa mboga hii kuonekana ni ya watu wenye kipato cha chini, lakini pia ina faida nyingi katika miili yetu.

Bamia husaidia kuondoa uchovu wa mwili pamoja na kusaidia kutibu tatizo la kukosa choo.

Aidha, bamia pia inaelezwa kusaidia kusafisha damu, kutibu mafua, vidonda vya tumbo, inaimarisha mifupa pamoja na kuwa kinga ya magonjwa kama utapiamlo na anemia.

Mboga hii imekuwa ni msaada kwa watu wenye matatizo ya mifupa au maumivu ya viungo kwani huongeza uteute kwenye viungo vya mifupa, ili upate faida hii inakupasa ule bamia kama supu.
Hizo ni baadhi ya faida za ulaji wa bamia, endapo utahitaji kufahamu mengine mengi tutafute kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com
Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment