Friday, 20 January 2017

Madhara ya kula nyama nyekundu na siku ngapi kwa wiki unaweza kula nyama hiyo


Kila chakula huwa na umuhimu wake ndani ya mwili lakini chakula hicho hicho huweza kuwa na mdhara pia.

Hivyo ndivyo ilivyo ndani ya nyama hasa nyama nyekundu yaani nyama ya ng'ombe na mbuzi licha ya kwamba nayo imesheheni sifa zake ikiwa ni pamoja na virutubisho kama protini na madini aina ya chuma lakini bado  inamadhara yake pia.

Miongoni mwa madhara ya nyama nyekundu ni pamoja na haya yafuatayo:-

1. Inaelezwa kuwa ulaji wa nyama nyekundu kwa kiasi kikubwa huchangia uwezekano wa saratani ya utumbo mkubwa.

2. Pia ulaji wa nyama nyekundu huchangia kudhoofisha mfumo wa umeng'enyaji chakula tumboni

3. Huongeza hatari ya magonjwa ya moyo.

4.Huongeza hatari ya kisukari (diabetes type 2)

Zingatia

Watalaam wanashauri kuwa kama ni lazima sana kwako kula nyama nyekundu basi angalau ndani ya wiki mzima mhusika ale nyama hiyo kwa kiwango kisichozidi nusu kilo.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment