Tuesday, 10 January 2017

Mambo manne ambayo yataongeza uzalishaji kwenye biashara yako


Ni wazi kwamba kuna wakati unaweza kujikuta unapoteza hamu kabisa ya kufanya kazi na hivyo kupelekea kushuka kwa uzalishaji mali ndani ya kampuni yako au biashara yako.

Hata hivyo, hali hiyo huweza kutokea mara chache sana, lakini pia hali hiyo unaweza kuondokana nayo kwa kufanya haya yafuatayo:-

1. Tenga majukumu yako ya siku katika ratiba maalum na jihakikishie kuwa huwezi kuondoka eneo lako la kazi hadi pale unapoyakamirisha yote.

2. Jaribu kuondoa vitu ambavyo vitakuondoa kwenye umakini wa kazi kama vile simu au kama inaumuhimu sana katika kazi yako basi unaweza kuiweka katika hali ya ukimya yaani silent ili isikuondolee umakini wa kazi zako.

3. Hakikisha kabla ya kufika ofisini au kwenye eneo lako la kazi basi tayari uwe na mpangilio wote wa majukumu yako ya siku husika yaani TO- DO - LIST.

4. Epuka kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja amua uanze na kipi kwanza na ukianza nacho hakikisha unamaliza ndio unaamia kwenye kazi nyingine na siyo kuchanganya kazi zaidi ya moja kwa wakati huo huo.

Kwa ushauri zaidi unaweza kutupigia kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment