Friday, 13 January 2017

Mambo manne yatakayolinda afya ya mapafu yako

Kuna baadhi ya mambo ambayo huwa tunafanya kila siku, lakini huenda yanachangia madhara fulani ndani ya afya ya mapafu yetu.

1. Kuepuka kuvuta sigaraa 
Sigara ni moja ya vitu ambavyo huchangia kwa kiasi kikubwa madhara ya mapafu ikiwa ni pamoja na saratani ya mapafu.

Moshi wa sigara huchangia kufanya njia ya hewa kuwa nyembamba na hivyo kufanya upumuaji kuwa mbaya.

Epuka kukaa na mtu anayevuta sigara pia

2. Fanya uchunguzi wa afya mara kwa mara
Uchunguzi wa afya wa mara kwa mara husaidia kupunguza uwezekano wa magonjwa mbalimbali, hata kama upo vizuri kiafya ni vyema ukajenga utamaduni huo wa kuchunguza afya yako.Wakati wa uchunguzi wa afya yako kwa kawaida mtaalam wa afya ataweza kusikiliza hali ya upumuaji wako.

3. Fanya mazoezi
Mazoezi ya mara kwa mara husaidia kuongeza utendaji kazi mzuri wa mapafu.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment