Thursday, 12 January 2017

Mambo matano yatakayokuepusha na magonjwa mara kwa mara


Baadhi ya watu si rahisi kwao kusikia wakiugua ugua. Sasa leo nataka tuzungumzia siri ambazo watu wasiougua mara kwa mara huzingatia.

1. Kulala kiasi cha kutosha
Watu wanaopata usingizi wa kutosha huwa na furaha na afya bora. Tafiti zinaonesha kwamba kupumzika na kupata usingizi kwa saa nane na zaidi ni muhimu katika kudumisha afya, kuzuia magonjwa na kukupa furaha.

2. Kufanya mazoezi
Mazoezi yana faida lukuki, ikiwa ni pamoja na kuzuia magonjwa sugu kama vile kisukari na magonjwa ya moyo. Mazoezi pia huongeza kinga ya mwili na kuongeza kiwango cha homoni zinazoleta hali ya furaha mwilini.

3. Zingatia ulaji wako
Chakula kinaweza kuwa dawa au sumu kwa maana ya kiasi na aina ya chakula. Hivyo kula chakula bora ni kitu muhimu katika kudumisha afya bora.

4. Dumisha furaha yako

Watu wanaotabasamu na kucheka mara kwa mara hujikinga na msongo wa mawazo hivyo kukaribisha furaha na afya katika maisha yao.

5. Zingatia usafi wa mikono yako

Tabia ya kunawa mikono mara kwa mara husaidia kuzuia magonjwa mbalimbali. Zaidi ni vyema kunawa kwa kutumia sabuni kwani hutukinga na magonjwa kama vile kuharisha na magonjwa ya tumbo.

Wataalamu wa afya wanashauri kunawa kabla na baada ya kula chochote, pia kunawa kila tunapotoka msalani na hata tunapotoka sehemu zenye mikusanyiko ya watu.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment