Saturday, 7 January 2017

Mambo matatu muhimu ya kuyajua kuhusu faida za mti wa muembe

Leo napenda tufahamishane kuhusu faida za embe, lakini pia pamoja na mazao yake mengine kama magome, majani, kokwa.

Zifuatazo ni baadhi ya faida za kiafya za mti wa mwembe

Tukianza na majani ya mti wa mwembe hususani yale machanga yanapochemshwa husaidia kutuliza maumivu ya tumbo, kupunguza hali ya kifua kikavu, homa pamoja na kuoshea vidonda na kusaidia vidonda kukauka haraka.

Aidha, unga wa majani hayo ya muembe pia hutumika katika kulinda afya ya meno endapo utatumika kwa kusukutua kinywani mara kwa mra.

Kingine zaidi ni kuhusu kokwa ambalo pia likiandaliwa vyema huweza kusaidia kuzuia tatizo la kuharisha.

Kuna mengi zaidi kuhusu mti huu wa mwembe, lakini si rahisi kuandika kila kitu hapa sasa ili kufahamu zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment