Monday, 2 January 2017

Matunda na viungo vyenye uwezo wa kuondoa mikunjo usoni kwa haraka

Kuanza kujitokeza kwa mikunjo usoni huwa ni dalili kuwa umri umesogea na mhusika anatoka kwenye utu uzima kuelekea uzeeni.

Hta hivyo, kwa sasa si jambo la ajabu kumkuta mtu anaumri wa miaka 20, lakini uso wake umeanza kukumbwa na mikunjo.

Zipo sababu kadhaa ambazo huweza kuchangia tatizo hili ikiwa ni pamoja na kukosa usingizi wa kutosha, kutokunywa maji ya kutosha pamoja na kusongwa na mawazo.

Sababu nyingine ni kutokula vyakula vyenye lishe bora pamoja na matumizi holela ya baadhi ya vipodozi.

Leo ninazo baadhi ya mbinu za kuondoa mikunjo usoni kwa wale ambao wameanza kupatwa na tatizo hilo:-

Kwanza unaweza kutumia juisi ya tango kwa kupaka sehemu zenye mikunjo (usoni) na kukaa kwa muda wa dakika zisizopungua 15 kabla ya kunawa kwa maji ya uvuguvugu. Hii unapofanya mara mbili kwa siku angalau itakusaidia kupunguza tatizo hilo na hata la madoa ya usoni kama yapo.

Njia nyingine ni kupata mchanganyiko wa papai na ndizi, ambapo utauchanganya vizuri kwa pamoja kisha paka taratibu usoni pasipo kusugua na utakaa baada ya dakika kadhaa kabla ya kunawa kwa maji ya uvuguvugu.

Pia unaweza kutumia kiazi ambacho kimesagwa kisha tumia kwa kupaka usoni na ni vyema zoezi hili likafanywa usiku kabla ya kulala ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Mbali na njia hizo pia unaweza kutumia mchanganyiko wa tangawizi pamoja na asali ambapo utasaga tangawizi kisha changanya kidogo na asali japo kijiko kimoja halafu tumia mchanganyiko huo kupaka usoni. Fanya hivyo angalau mara moja kila siku na utaona mabadiliko.

Zipo njia nyingi nyingine za kukufanya kuwa katika muonekano mzuri, lakini kwa maelezo zaidi unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani

No comments:

Post a Comment