Tuesday, 10 January 2017

Mbinu za kumaliza tatizo la kutokwa na maji yenye harufu sehemu za siri

Picha kwa msaada wa mtandao

Jambo la kutokwa na majimaji meupe yasiyo na rangi wala harufu mbaya katika sehemu za siri (ukeni) ni jambo la kawaida kwa wasichana na wanawake na wala si jambo geni

Tatizo linakuja pale ambapo majimaji hayo yanapokuwa yanatoka mengi sana kiasi cha kuchilizika mapajani na kulowanisha kabisa nguo za ndani, hali hiyo yaweza kuwa sio ya kawaida.

Majimaji ya ukeni yanayowasha au kuwa na harufu mbaya au yaliyoganda kama maziwa ya mgando au tui la nazi yanatokana na uambukizo wa fangasi au kisonono.

Tatizo hili kwa kiasi kikubwa huweza kuchangia harufu mbaya sehemu za siri kutokana na kushambuliwa na bakteria wanaokaa na kuzaliana kwenye ngozi yenye unyevunyevu mwingi

Kwa mwanamke ambaye anasumbuliwa na shida hii mara nyingi hana budi kunawa mara kwa mara na sabuni isiyokuwa na kemikali na kujikausha na kitambaa safi pamoja nakuvaa nguo za ndani zenye asili ya pamba na kubadili mara kwa mara.

Pia mwanamke mwenye tatizo hili anapawa kuepuka kuvaa nguo za ndani zinazobana sana na zile zilizotengenezwa kwa kitambaa cheusi cha nguo aina ya polyster hasa katika maeneo ya joto jingi.

Pamoja na hayo, mwanamke mwenye shida ya kutokwa maji sehemu za siri ni lazima azingatie utunzaji wa mazingira ya sehemu zake za siri ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usafi wa nywele za siri na muda wote ziwe fupi.

Ili kupunguza tatizo la muwasho sehemu za siri jitahidi sana kunywa maji ya kutosha na juisi za matunda kwani huweza kusaidia kutuliza matatizo hayo ya muwasho.

Mbali na hayo unashauriwa kufika kwenye kituo cha afya ambacho kipo karibu na wewe ili kupata ushauri zaidi au matibabu endapo utakuwa unasumbuliwa na shida hii.

Pia unaweza kutupigia sisi kwa simu namba 0716 300 200 / 0784 300 300/ 0769 400 800 kwa ushauri zaidi.

Kumbuka kuwa ushauri huu umeletwa kwako chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania (WUTA) shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kupambana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment