Thursday, 26 January 2017

Miguu yako inavyoweza kukupa ukweli wa afya yako

woman holding red shoes
Ni nadra sana wengi wetu kujali kuhusu miguu wengi tunapopatwa na matatizo kwenye miguu huwa hatuwekei maanani sana.

Lakini ukweli ni kwamba miguu huweza kutueleza baadhi ya matatizo kadhaa ndani ya miili yetu.

Miongoni mwa matatizo ambayo huweza kuoneshwa kwa kupitia miguu ni pamoja na haya:-

1. Ubaridi kwenye miguu.
Hali hii inapojitokeza huashiria dalili za mzunguko hafifu wa damu ndani ya mwili au dalili za shinikizo la damu au kisukari n.k. Hivyo unapohisi hali hiyo ni vyema kuwaona wataalam wa afya kwa ushauri zaidi.

2. Maumivu ya miguu
Hii nayo si dalili nzuri kwani huweza kuwa ni dalili ya uwepo wa ufa mdogo kwenye mifupa au kwa wale wanaofanya mazoezi huweza kuwa ni dalili za kuwa mazoezi unayofanya ni makali zaidi, lakini pia kwa wanawake ambao hupenda kuvaa viatu virefu huweza kuwa ni sababu pia. Hivyo ni vyema kuyaangalia yote hayo katika kukabiliana na tatizo hili.

3. Miguu kuvimba
Tatizo hili huweza kuchangiwa endapo mhusika anafanya shughuli za kusimama muda mrefu, lakini pia tatizo hili huwatokea zaidi kinamama hasa wakati wa ujauzito, huku sababu kubwa mara nyingi ikiwa ni uwepo wa mzunguko hafifu wa damu ndani ya mwili  pamoja na dalili za matatizo ya figo.

4. Miguu kuwaka moto
Tatizo hili mara nyingi huwatokea zaidi wale wenye kisukari, lakini pia huweza kuchangiwa na ukosefu wa vitamin B au matatizo sugu ya figo pamoja na mzunguko hafifu wa damu.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment