Wednesday, 11 January 2017

Nimekuwekea hapa dalili 3 za upungufu wa maji kwa mtoto wako

Mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo haja ndogo pamoja na jasho hali hiyo huweza kuchangia mhusika kukumbwa na upungufu wa maji mwilini.

Inaelezwa kwamba karibu theluthi mbili ya miili yetu imejaa maji, lakini leo natapenda kuzungumza juu ya tatizo hili kwa upande wa watoto na tutaangalia dalili zake.

1. Kupata haja ndogo kwa shida au kutopata kabisa.

2. Mtoto kukosa uchangamfu

3. Kukauka kwa midomo.

4 . Mtoto kulia mara kwa mara, huku machozi yakigoma kutoka au kutoka kidogo sana

Tatizo hili huweza kujitokeza endapo mtoto atakuwa anatapika au kuharisha yote hayo huweza kuchangia kupoteza maji mengi. 

Wahi kituo cha afya kilichokaribu na wewe ili kupata huduma za haraka endapo mtoto ataendelea kuwa na hali mbaya kutokana na hili ikiwa ni pamoja na kupoteza nguvu.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Kumbuka kuwa ushauri huu umeletwa kwako chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania (WUTA) shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kupambana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.

No comments:

Post a Comment