Monday, 9 January 2017

Nimekuwekea hapa maelezo na video kuhusu umuhimu wa komamanga kiafya


Mwenyezi Mungu ametujalia aina mbalimbali za matunda ambayo yote yamekuwa yakitupatia faida lukuki ndani ya miili yetu.

Leo napenda tuambiane kuhusu faida hizi za komamanga kiafya.

1. Komamanga husiadia kutukinga dhidi ya saratani
Uwezo huo unatokana na kuwa na vitamin A, C pamoja na madini ya chuma ambayo kusaidia kukinga dhidi ya saratani ya kibofu, mititi pamoja na saratani ya mapafu.

2. Huongeza kinga za mwili
Hii ni kwasababu tunda hili limesheheni vitamin C kwa zaidi ya asilimia 15 ya vitamin hiyo inayohitajika ndani ya miili yetu kila siku na hivyo kulifanya kuwa tunda muhimu hasa katika kuimarisha mfumo wa kinga ndani ya mwili.

3. Humiarisha afya ya mifupa
Unapotumia komamanga mara kwa mara husaidia kuimarisha afya ya mifupa pamoja na kuzuia maumivu ya misuli ya mara kwa mara.

4. Hupunguza uzito
Hii ni kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha nyuzi nyuzi ambacho husaidia kudumisha uzito unaofaa.

5.Huzuia uharibu wa seli mwilini
Hii ni kwa sababu tunda hili linakirutubisho kiitwancho anti- oxidants ambacho husaidia kuzuia uharibufu wa seli mwilini.

Hizo ni faida tano za komamanga kama ungependa kufahamu faida nyingine zaidi kuhusu tunda hili unaweza kutazama video hii hapa chini;-


Kwa maelezo zaidi au ushauri unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment