Thursday, 5 January 2017

Sababu 5 zinazochangia kuvuruga mzunguko wako wa hedhi kila mwezi

Naamini wengi tunafahamu kuwa mwanamke anapopata ujauzito huwa hazioni siku zake za hedhi 

Lakini kuna wakati mwingine mwanamke anaweza kuwa si mjamzito na bado akajikuta anashindwa kuona siku zake za hedhi.

Zipo sababu kadhaa ambazo huweza kuchangia hali hiyo kujitokeza:-

1. Kwanza maambukizi
Maambukizi haya yanaweza kuwa ni ya magonjwa fulani ambayo huweza kuchangia kuvuruga mfumo wa utoaji hormone katika mwili wa mwanamke.

2. Ulevi
Matumizi ya vileo huweza kuwa chanzo pia cha tatizo hili na athari huweza kuwatokea zaidi wanawake walio kati ya umri wa miaka 25 hadi 49.

3. Matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango
Baadhi ya njia za uzazi wa mpango huwafanya baadhi ya wanawake kukosa hedhi kwa kipindi kirefu au kujikuta wakiwa na mzunguko mbovu wa hedhi. Hali hii hutegemea pia kati ya mtu na mtu.

4. Hali ya uzito mkubwa
Wanawake wengine hukumbwa na tatizo hilo kutokana na kuongezeka uzito. Imethibitika kuwa uzito ukiwa mkubwa kwa wanawake unasababisha kuingia katika hatua za kuacha kupata hedhi kwa kuchelewa kwa mwaka mmoja zaidi ikilinganishwa na wanawake ambao hawana uzito mkubwa.

5. Hata hivyo, ni vyema ikafahamika kuwa kwa kawaida mwanamke huweza kuacha kupata hedhi (Menopause) mara anapofikisha umri kati ya miaka 42 -55 na kuendelea.

Zingatia.
Mwanamke unapoona dalili au kutopata hedhi yako kwa muda muafaka ni vyema ukaenda kumuona daktari ili kufanya uchunguzi wa tatizo hilo mapema.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment