Wednesday, 25 January 2017

Sababu 7 za kukosa hisia za kushiriki tendo la ndoa


Wanamke kadhaa wamekuwa wakiwasiliana nasi na kuuliza kuhusu kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa, tatizo ambalo huenda likawa kwa wanawake wengi na baadhi yao hushindwa kusema tu.

Hata hivyo, wanawake wengi ambao husumbuliwa na tatizo hili muda mwingi hujikuta wakiutumia kupiga stori zaidi na wenzao tu au kutembelea mitandao ya kijamii huku wakichati na marafiki karibu siku nzima na huo ndio huwa utaratibu wao wa kila siku.

Zifautazo ni sababu zinazoweza kuchangia tatizo la mwanamke kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

Suala la kisaikolojia
Tendo la ndoa hutegemea sana hisia, hivyo ikiwa mwanamke amewahi kukumbwa na matatizo yaliyochangia kumuathiri kisaikolojia ikiwa ni pamoja na matukio ya ubakaji, mawazo mengi hasa ya kazi, matatizo ya kifedha, kutojiamini na kuhisi labda maumbile yake mwanamke hayavutii basi mwanamke huyo huweza kupatwa na tatizo hilo.

Matatizo ya kimahusiano
Ni ngumu sana mwanamke kushiriki tendo la ndoa na mwanaume ambaye hana hisia naye, hii ipo tofauti kwa wanaume ambao wao huweza kushiriki tendo hilo hata kwa mwanamke asiyekuwa na hisia naye kabisa na akashiriki vizuri tu, lakini hiyo ni nadra sana kutokea kwa wanawake labda ikiwa ni mfanyabiashara wa ngono. Hivyo kama mwanamke atakuwa hana mahusiano imara basi huweza kujikuta akiingia kwenye tatizo hili.

Kuhisi maumivu
Ikiwa mwanamke huhisi maumivu makali wakati wa cha kufanya tendo la ndoa basi nayo huweza kuwa sababu ya mwanamke kupoteza hamu kabisa ya kushiriki tendo hilo.

Matumizi ya baadhi ya dawa
Kuna baadhi ya dawa huweza kuchangia tatizo hili, hivyo ni vizuri kabla ya kutumia dawa yoyote mwanamke akahakikisha amepata ushauri kutoka kwa wataalam wa afya ili kuepuka tatizo hilo.

Magonjwa
Hii nayo huweza kuwa sababu ya tatizo hili, kwani baadhi ya magonjwa huweza kupelekea hata mhusika kukosa hamu kabisa ya tendo la ndoa. Mfano maumivu ya viungo, maumivu ya tumbo, kisukari au presha n,k

Kunyonyesha au ujauzito
Homoni huweza kuwa tofauti pale mwanamke anapokuwa katika nyakati hizi na kuweza kuchangia kukosa hamu ya tendo hilo, hivyo mwanamke hujikuta akihitaji msaada mkubwa kutoka kwa mwenzi wake ili kuwa katika hali ya kawaida.

Umri
Kwa kawaida kadri umri unavyozidi kwenda hamu ya kufanya tendo la ndoa nayo hupungua kwa wanawake na mwanamke anapofika miaka 45 au 50 mwanamke huweza kuingia kwenye kipindi cha kukoma kwa hedhi 'menopause' ambapo homoni inayoitwa oestrogen hupungua sana na kumfanya kuhisi kwa tabu sana hisia za tendo hilo.

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment