Sunday, 29 January 2017

Unga wa karafuu & mafuta ya ufuta jinsi vinavyoweza kumaliza maumivu ya sikio


Sikio, pua na koo ni moja ya viungo ambavyo vinaukaribu sana ndio maana pale kimojawapo kinapopatwa na tatizo huweza kuchangia tatizo kwa kiungo kingine pia.

Hata hivyo, hapa nahitaji kueleza kuhusu maumivu ya sikio na namna ya kumaliza ukiwa nyumbani kwako.

Maumivu ya sikio huweza kusababishwa na jipu au upele ndani ya njia ya sikio, kelele za nguvu, kupeng'a kamasi kwa nguvu, kukauka kwa nta ndani ya sikio pamoja na sababu nyingine.

Pamoja na hayo, kama nawe pia unamaumivu ya sikio basi unaweza kutumia karafuu.

Tafuta karafua  kisha chukua unga wake, kisha changanya kijiko kimoja cha chai cha mafuta. Baada ya hapo weka matone matatu ya mchanganyiko huo katika sikio mara mbili kwa siku kwa muda wa siku tano.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment