Tuesday, 10 January 2017

Usipozingatia mambo haya basi tegemea kuharibika kwa meno ya mwanao


Tatizo la kuoza kwa meno ni moja ya tatizo ambalo huwakumba watoto wengi katika kipindi cha ukuaji wao.

Mbaya zaidi tatizo hili husababisha watoto wengi meno kushambuliwa kwa mpigo hasa kuanzia meno ya juu na mbele.

Katika tatizo hili mara nyingi meno ya chini na mbele ni mara chache kushambuliwa kwa kutokana na kukingwa na visababisha vya kuoza na ulimi.

Kuna baadhi ya sababu zinazochangia kuoza kwa meno kwa kasi katika kipindi cha utoto sababu hizo ni pamoja na tabia ya ulaji ya mtoto (feeding habits). Watoto wengi hupenda kunywa vinywaji vyenye sukari kwa muda mrefu na mara nyingi.

Watoto walio kwenye hatari zaidi ya kuoza kwa meno ni wale wa watoto wa wazazi wenye shughuli nyingi na hivyo kulazimika watoto kutumia chupa za kufyonzea kwa muda mrefu ambao hawapo nao. Pia watoto wenye kutumia dawa zenye sukari mara kwa mara.

Hali kadhalika watoto wale ambao huachishwa kunyonya mapema zaidi huwa katika hatari ya kuoza kwa meno kutokana na kutumia chupa kama mbadaala wa zoezi hilo.

Mzazi unapaswa kujenga utaratibu wa kumkagua mtoto wako kinywa mara kwa mara na unapoona tatizo ni vyema ukampeleke hospitali mapema.

Pia mzazi unashauriwa kudhibiti matumizi ya vinywaji na vitu vya sukari mara kwa mara.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment