Thursday, 26 January 2017

Vyakula & vinywaji vyenye uwezo wa kuongeza uwezo wa kufikiri harakaHabari za leo mdau wa tovuti hii, najua kwa sasa wengi tumezongwa na majukumuu kadhaa hasa ya kutafuta mkate wa kila siku kwahiyo kuna wakati unaweza kufanya kazi au kufikiria sana na kujikuta kama akili yako  imefika mwisho kabisa wa kiwango cha kufikiri.

Sasa hapa napenda kukwambia kuhusu aina ya vyakula na vinywaji ambavyo huweza kuongeza uwezo wa kufikiri kwa haraka.

Mua.
Kwa kawaida mua huwa na sukari asili yenye uwezo wa kuongeza nguvu ndani ya mwili, hivyo unapohisi kuchoka au kushuka kwa uwezo wako wa kufikiri unaweza kunywa japo juisi ya mua na baada ya muda utaona unarejea kwenye hali yako ya kawaida na kuweza kuendelea na kazi zako.

Unywaji wa chai
Tafiti zinaonesha kuwa watu ambao hupata kifungua kinywa huwa na uwezo mzuri wa kufikiri zaidi ya wale ambao huamka asubuhi na kuanza shughuli zao au watoto  kwenda shule pasipo kupata chai. Hivyo ni vyema kujenga utaratibu wa kunywa chai asubuhi kabla ya kuanza shughuli zako.

Ulaji wa samaki.
Matumizi ya kitoweo hiki nayo ni muhimu kwa afya ya akili kutokana na samaki kuwa na kitu kiitwacho Omega 3 ambayo ni muhimu pia kwa afya ya akili.

Pia matumizi ya kitoweo hiki husaidia hata kwa wazee kurejesha uwezo wa kumbukumbu zao vizuri.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment