Thursday, 26 January 2017

Zifahamu dalili za awali kabisa za pumu

Boy Having Asthma Attack
Pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu yaani mirija myembamba ya hewa zinazofahamika kitaalam kama 'bronchi oles'

Hali ambayo humfanya muathirika kushinwa kuvuta hewa nje na hivyo kupumua kwa shida, lakini tatizo hili huweza kudumu kwa muda mfupi au muda mrefu kiasi cha kuhitaji huduma ya kwanza au tiba.

Hata hivyo zipo dalili za awali kabisa za tatizo hili ambazo ni vyema ukazifahamu leo kupitia tovuti hii ya www.dkmandai.com.

1. Kukohoa sana hasa wakati wa usiku

2. Kupata tabu wakati wa kulala usiku.

3. Pumzi kukata mara kwa mara.

Pale tatizo linapokuwa limeanza kukomaa kabisa ndio utaanza kuhisi sauti kama ya mluzi kifuani pamoja na pumzi kubana zaidi.

Hivyo basi unapoona dalili hizo tambua kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa upo njiani kukumbwa na tatizo hili la pumu.

Kwa maelezo zaidi tupigie kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 tutakushauri na ukusaidia kumaliza tatizo hilo bila shida.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment