Monday, 27 February 2017

Ahsante kwa wale wote waliofika kwenye mafunzo haya

Keki iliyoandaliwa na washiriki waliofika kwenye mafunzo ya ujasiriamali tarehe 25/02/2017
Siku ya tarehe 25/02/2017 ilikuwa siku muhimu kwa baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la THE WORK UP TANZANIA kwa kushirikiana na Mandai Products Co (T) Ltd.

Semina hiyo ambayo ilihusu utengenezaji wa mkate , keki, tomato sauce na tomato sauce pamoja na namna ya kuanza biashara na kuendeleza biashara yako.

Hapa nimeona nikuwekee baadhi ya picha kutoka kwenye semina hiyo zikionesha matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea:

Mmoja wa washiriki akikoroga ice sugar tayari kwaajili ya kupamba keki iliyoandaliwa kwenye mafunzo hayo

Mwalimu Rose Mehena akimimina mayai kwenye ice sugar tayari kwa ajili ya kupamba keki iliyoandaliwa siku hiyo
Keki ikiwa katika harakati za kupambwa
Mwalimu Rose Mehena akisisitiza jambo kwa washiriki kuhusu namna ya kupamba keki

Keki ikiwa katika hatua za mwisho kuelekea kukamilika

No comments:

Post a Comment