Tuesday, 7 February 2017

Aina 5 ya matunda ambayo husaidia kupunguza unene haraka


Leo naomba nikusogezee aina hizi za matunda ambayo yakitumiwa mara kwa mara huweza kusaidia kupunguza uzito mkubwa.

Naomba nikuorodheshehe matunda hayo hapa ili kama utapenda kuyatumia uweze kuchangua utapenda kutumia matunda ya aina gani:-

1. Tikiti Maji
watermelon
Hii ni kwa sababu asilimia 90 ya tunda hili ni maji, hivyo ni moja kati ya matunda ambayo huingia kwenye orodha ya kuweza kupunguza uzito mwilini.

2. Pera
guavas
Pia ni miongoni kati ya matunda yenye uwezo wa kupunguza uzito wa mwili kutokana na kuwa na nyuzinyuzi pamoja na virutubisho kadhaa.

3. Ndizi
bananas
Ni tunda lenye ladha ya sukari ya asili na isiyo na madhara mwilini, nalo pia huweza kusaidia kupunguza uzito likitumika vizuri.

4. Apple/ Tufaa
apple
Ni miongoni kati ya matunda ambayo huweza kupunguza uzito wa mwili kwa haraka ikiwa litatumika mara kwa mara au kuandaliwa kama juisi.

5.Nyanya
tomato
Nyanya pia ni miongoni mwa matunda yenye uwezo wa kupunguza uzito wa miili yetu endapo litatumika ipasvyo.

Kwahayo machache naomba niishie hapo, lakini kwa mengine mengi zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment