Wednesday, 1 February 2017

Dalili za awali za matatizo ya ini & jinsi ya kupambana na tatizo hilo


Homa ya ini ni ugonjwa unaotokana na virusi  na kitaalam ugonjwa huu hufahamika pia kama Hepatitis B.

Wataalam wa afya wanaeleza kuwa ugonjwa huu huweza kuambukizwa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujamiana pasipo kutumia kinga, mapenzi kwa njia ya mdomo pia mama mjamzito anaweza kumuambukiza mtoto wakati wa kujifungua.

Ugonjwa huu pia huweza kuenezwa kwa kuchangia damu pamoja na vitu vyenye ncha kali na hata miswaki.

Zifuatazo ni dalili za ugonjwa wa ini.

1. Kuhusi uchovu na wakati mwingine kutapika.

2. Homa kali na mwili kuwa dhaifu

3. Ngozi na macho kubadilika rangi na kuwa ya njano

4. Kupoteza hamu kula

5. Rangi ya mkojo kubadilika na kuwa nyeusi.

Dalili nyingine ni maumivu makali ya tumbo hasa upande wa ini

Miongoni mwa mbinu za kukabiliana na ugonjwa huo ni pamoja na kupata chanjo, kujikinga kwa kutumia kinga wakati wa kujamiana na kuepuka kutumia vitu vyenye ncha kali kama sindano n.k.

Namna  ya kulinda afya ya ini lako;-
1. Acha kabisa matumizi ya pombe.

2. Acha mara moja uvutaji wa sigara.

Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba:- 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha matumizi ya lishe bora. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.

No comments:

Post a Comment