Wednesday, 8 February 2017

Fahamu faida za majani ya mapindigesi 'peaches' kiafya


Mapindigesi au 'peaches' kama yanavyofahamika kwa lugha ya kingereza ni tunda ambalo limekuwa likipatikana sana katika mikoa ya nyanda za juu kusini ikiwa ni pamoja na Iringa lakini pia mbali na mikoa ya nyanda hizo hata Tanga pia tunda hili hupatikana.

Kama utakuwa ni msomaji wa tovuti hii mara kwa mara naamini utakumbuka kuwa hivi karibuni tulieleza kuhusu umuhimu wa mapindigesi 'peaches''

Leo naomba kukueleza kuhusu faida za majani ya mti wa mapindigesi 'peaches'

Majani hayo husaidia kutuliza matatizo kadhaa ya kiafya ikiwa ni pamoja na maumivu ya kichwa, koo na hata kichefuchefu.

Aidha, majani hayo pia husaida kutatua matatizo ya mkojo, kukosa usingizi, kikohozi pamoja na maradhi ya tumbo.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Ushauri huu umetolewa chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la The Work Up Tanzania (WUTA) ambalo linadhamira ya dhati ya kupambana na umasikini, ujinga na maradhi kwa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya lishe bora zitokanazo na mimea na matunda. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment